Kozi hii inahusika na mbinu na matumizi ya Kiswahili kwa ujumla, lakini inatilia mkazo zaidi uandishi, shabaha kuu ikiwa ni makosa ya kijumla na mahususi ya uandishi wa habari za Kiswahili katika vyombo mbalimbali kama vile televisheni, redio, na magazeti. Makosa ya kijumla yanayoshughulikiwa ni ya kimpangilio na kimtiririko; na makosa mahususi yanahusiana na kanuni za utamkaji wa maneno, uumbaji wa maneno, uundaji wa sentensi na aya, uteuzi wa msamiati, ukataji na uendelezaji maneno pamoja na utumizi wa viakifishi na alama nyingine za uandishi. Madhumuni makuu ni kuwawezesha washiriki kukuza stadi za uandishi, na hususani matumizi fasaha ya lugha, katika aina zake mbalimbali.
KEY TOPICS
By the end of the course participants will be able to:
Kutokana na ukweli kwamba kukua na kupanuka kwa matumizi ya Kiswahili kumeenda sambamba na kuzuka kwa makosa mengi ya kisarufi na kimantiki yanayoathiri ubora wa habari katika vyombo husika, kozi hii inawalenga wanahabari wote, wakiwamo waandishi, watangazaji na wahariri kutoka vituo vya runinga, redio, magazeti ya Kiswahili na waendeshaji wa blogu mbalimbali. Kwa kuzingatia kwamba baadhi ya wanahabari ni waajiriwa na kwamba muda wa asubuhi wanakuwa kazini kozi hii itafundishwa kwa mtindo wa mwendokasi siku tano za kazi kuanzia saa 10 alasiri hadi saa 1 usiku kwa majuma matatu.
Offered By : Kiswahili Language -
Institute of Kiswahili Studies
Cost: 500,000